Lugha Nyingine
China yaongeza uwekezaji katika mawasiliano ili kustawisha uchumi
Picha iliyopigwa tarehe 26, Agosti, 2022 kutoka angani ikionesha sehemu ya barabara ya mwendo kasi kutoka Yuxi mpaka Chuxiong huko Yunnan, Kusini Magharibi mwa China. (Xinhua/Jiang Wenyao)
Kutoka ujenzi wa barabara mpya ya mwendo kasi hadi kukarabati njia ya usafirishaji wa meli, China imepanua na kuboresha mtandao wa mawasiliano mwaka huu, ili kuchochea uwekezaji na kuhimiza maendeleo.
Msemaji wa habari wa Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi ya China Shu Chi Jumatano wiki hii kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema kuwa, ujenzi wa miradi mikubwa ya mawasiliano unaendelea vizuri mwaka huu, na umechangia uwekezaji kwa nguvu.
Kuanzia Januari hadi Agosti, uwekezaji wa mali isiyohamishika wa sekta ya mawasiliano na uchukuzi umeongezeka kwa asilimia 6.6 ukilinganishwa na wakati kama huo wa mwaka jana, ukifikia Yuan trilioni 2.34 (Dola za Marekani bilioni 329 hivi). Uwekezaji huo umechangia sana ufufukaji wa uchumi wakati China inapokabiliwa na changamoto mbalimbali nchini na nje ya nchi.
Wachambuzi walisema, katika hali ya kudumisha mwelekeo wa ongezeko la uchumi, uwekezaji wa mawasiliano utafanya kazi ya kuchangia kupanua uwekezaji wenye ufanisi, kujitahidi kuongeza nafasi za ajira na kutuliza uchumi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma