Lugha Nyingine
Rais Xi atuma barua ya pongezi kwa Maonesho ya 7 ya China-Eurasia yaliyofunguliwa Urumqi, Xinjiang (5)
Picha iliyopigwa Septemba 19, 2022 ikionyesha moja ya banda kwenye Maonesho ya Saba ya China-Eurasia huko Urumqi, Mji Mkuu wa Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur, Kaskazini Magharibi mwa China. Maonyesho ya Saba ya China-Eurasia yamefunguliwa hapa Jumatatu. Yakichukua eneo la maonyesho lenye ukubwa wa mita za mraba 40,000, maonyesho hayo yamewekwa maeneo matatu yanayoonesha mada kuhusu uwekezaji, ushirikiano na biashara ya bidhaa. (Xinhua/Li Xiang) |
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametuma barua ya pongezi kwa Maonesho ya Saba ya China-Eurasia, yaliyofunguliwa Jumatatu huko Urumqi, Mji Mkuu wa Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur, Kaskazini Magharibi mwa China.
“Likiwa na uhai na uwezekano wa maendeleo, Bara la Eurasia ni eneo muhimu kwa ushirikiano wa kimataifa katika ujenzi wa pamoja wa ‘Ukanda Mmoja, Njia Moja’,” Xi amesema kwenye barua yake.
Xi amesema, katika miaka ya hivi karibuni, Xinjiang ya China imetoa mchango ipasavyo kwa kutumia nguvu bora ya eneo lake ili kuendeleza kikamilifu ujenzi wa eneo la msingi la Ukanda wa Kiuchumi wa Njia ya Hariri na kuhimiza muunganisho, ushirikiano wa kunufaishana na maendeleo ya pamoja kati ya China na nchi za Eurasia, na matunda mazuri yakiwa yamepatikana.
Amesisitiza kuwa, China inapenda kushirikiana na nchi nyingine kuhimiza moyo wa Njia ya Hariri unaojumuisha amani na ushirikiano, uwazi na shirikishi, kufundishana na kuigizana, na kunufaisha kwa pamoja, huku Maonesho ya China na Eurasia yakiwa ni jukwaa.
“Wakati huo huo, China iko tayari kushirikiana na nchi nyingine kutafuta maendeleo ya hali ya juu na ya endelevu, ambayo yatawanufaisha watu, na kupanua sekta za ushirikiano wa Eurasia, kuinua ushirikiano katika ngazi mpya, na kuhimiza maendeleo na ustawi wa pamoja.
Maonyesho hayo yameandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Biashara ya China, Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Baraza la China la Kuhimiza Biashara ya Kimataifa, na Serikali ya Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur.
Mapacha wa simba wachanga walioachwa na mama yao wakua vizuri
Shule zarejesha masomo katika maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi huko Luding, Sichuan
Moto wa misituni waenea kwa kasi na kutishia wakazi wengi huko California, Marekani
Wanafunzi wapata lepe kwenye viti vinavyoweza kubadilika huko Chongqing
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma