久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Kenya yasema shehena ya kwanza ya parachichi imeingia kwenye soko la China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 29, 2022

NAIROBI - Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Kutangaza Bidhaa na Chapa za Kuuzwa Nje za Kenya (KEPROBA) Wilfred Marube amesema jana Jumapili kuwa, shehena ya kwanza ya parachichi kutoka Kenya imeingia katika soko la China.

Marube amesema kuingia kwa parachichi kwenye soko la China ni ushindi mkubwa kwa Kenya kwa sababu kutasaidia kuvuta ukuaji wa uchumi wa Kenya kupitia biashara ya kimataifa ya parachichi.

"Majaliwa ya uzalishaji yanapendelea Kenya. Kwa kuwa na idadi kubwa ya watu, mauzo ya nje kwenda China pia yatawezesha kuongezeka kwa mapato ya fedha za kigeni pamoja na ajira kwa vijana wa kike na wa kiume," Marube amesema katika taarifa yake aliyoitoa Nairobi, Mji Mkuu wa Kenya.

Amesema kuwa usafirishaji wa parachichi kutoka Kenya hadi China ulianzia Mwaka 2018 kwa kusaini makubaliano kadhaa baina ya nchi mbili (MoUs) inayoruhusu ufikiaji wa soko kwa bidhaa za kilimo za Kenya.

Kenya ilianza kusafirisha parachichi hadi nchini China Agosti 2 mwaka huu kufuatia kutekelezwa kwa makubaliano yaliyosainiwa kuhusu mahitaji ya usafi wa mazao mabichi kwa mauzo ya nje ya nchi hiyo. Hii ilifuatia ziara rasmi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi nchini Kenya mwezi Januari mwaka huu.

Marube ameeleza kuwa takriban makampuni kumi yamefuata viwango vilivyowekwa na yameidhinishwa kusafirisha parachichi safi kwenda China.

Balozi wa Kenya nchini China Muthoni Gichohi ambaye hivi majuzi alishiriki kwenye hafla rasmi ya kukabidhiwa shehena ya kwanza ya parachichi kutoka Kenya hadi Beijing, Mji Mkuu wa China, amepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali za Kenya na China katika kufikia mafanikio hayo.

Gichohi alithibitisha kujitolea kwa Kenya kusaidia jumuiya za wafanyabiashara katika nchi zote mbili wakati ambapo zinatarajia kuimarisha urahisishaji wa biashara na pia ufikiaji wa soko kwa bidhaa na huduma zao.

Takwimu za Serikali ya Kenya zinaonyesha kuwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki inauza nje wastani wa tani 80,000 za parachichi kila mwaka, huku masoko makuu kwa miaka mingi yakiwa ni nchi za Umoja wa Ulaya na Mashariki ya Kati.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>