Lugha Nyingine
Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China asema, “Soko la China bado linavutia uwekezaji wa kigeni”
Picha iliyopigwa Septemba 30, 2020 ikionyesha mandhari ya mtaa wa eneo la Lujiazui, Pudong, Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua/Wang Xiang)
BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China, Shu Jueting Alhamisi wiki hii amesema kuwa, soko la China bado linaendelea kuvutia uwekezaji wa kigeni, huku kukiwa na ukuaji unaoendelea wa uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDIs)
FDIs inayoingia China Bara, katika matumizi halisi, iliongezeka kwa asilimia 17.3, hadi kufikia yuan bilioni 798.33 katika miezi saba ya kwanza ya mwaka huu kuliko ile ya kipindi kama hiki cha mwaka jana. Kwa masharti ya dola za Marekani, mapato yatokanayo na uwekezaji wa kigeni yaliongezeka kwa asilimia 21.5 hadi kufikia dola bilioni 123.92 za Marekani.
Msemaji Shu wakati akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, amehusisha kuvutia kiuchumi kwa China na mambo manne.
“Umaalumu wa China, ikiwa ni pamoja na mfumo kamili wa viwanda, soko la hali ya juu zaidi, utulivu wa kijamii, na misingi mizuri ya kiuchumi katika muda mrefu, umetengeneza msingi mzuri wa maendeleo ya makampuni yanayowekezwa kwa mtaji wa kigeni,” Shu amesema.
Ameeleza kuwa, soko la China linalofunguliwa daima linatoa fursa zaidi, na uboreshaji thabiti wa mazingira yake ya biashara unaimarisha imani kwa kampuni za kibiashara za kigeni.
Shu amesema, China ilitekeleza orodha mpya hasi kwa uwekezaji wa kigeni ili kupanua zaidi ufikiaji wa soko lake. Pia ilifuta, kurekebisha au kutunga kanuni 520 ili kuboresha mazingira ya kisheria kwa uwekezaji wa kigeni, na kuongeza juhudi za kulinda haki na maslahi halali ya kampuni za kibiashara za kigeni.
“Kazi pia imefanywa kusaidia kushughulikia shida zinazokabili kampuni za kibiashara za kigeni,” Shu amesema, huku akitoa mfano wa juhudi za serikali kusaidia kampuni hizi kuanza tena uzalishaji wakati wa janga la UVIKO-19.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma