Lugha Nyingine
Sarafu ya Euro yadondoka chini ya usawa dhidi ya dola ya Marekani kwa mara ya pili mwaka huu (3)
Picha iliyopigwa Agosti 22, 2022 ikionyesha sanamu ya nembo ya Euro huko Frankfurt, Ujerumani. |
FRANKFURT – Sarafu ya Euro Jumatatu wiki hii ilishuka chini ya usawa dhidi ya dola ya Marekani kwa mara ya pili mwaka huu huku wasiwasi wa kuzorota kwa mgogoro wa nishati na kukazwa zaidi kwa sera za kifedha za Marekani ukizidi.
Hadi kufikia saa 5:22 asubuhi kwa saa za Ulaya, sarafu ya euro ilikuwa ikiuzwa kwa dola 0.9953 katika soko la sarafu na kufikia kiwango chake cha chini kabisa tangu katikati mwa Julai.
"Thamani halali ya euro imeharibiwa na mshtuko wa nishati", anasema Chris Turner, mkuu wa masoko wa kimataifa katika taasisi ya fedha ya kimataifa ING.
Uwezekano wa kutokea mgogoro wa gesi ulifunika ukanda wa sarafu ya euro, limeandika gazeti la Ujerumani Handelsblatt, na kuongeza kuwa wawekezaji wanaendelea kuwa na wasiwasi kuhusu uamuzi wa kampuni kubwa ya nishati ya Russia, Gazprom kusitisha usambazaji wa gesi asilia kwenda Ulaya kupitia bomba la Nord Stream 1 wakati wa ukarabati unaodumu kati ya Agosti 31 na Septemba 2.
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Ujerumani ARD, sababu nyingine ya udhaifu mpya wa euro ni sera ya viwango vya riba ya Benki Kuu ya Marekani. Wawekezaji kadhaa kwa sasa wanatarajia Benki Kuu ya Marekani itaongeza viwango vya riba tena kwa pointi 75 za msingi Septemba 21.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma