Lugha Nyingine
Ushirikiano wa uchumi na biashara wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” waongezeka katika sekta ya viwanda visivyochafua mazingira na utengenezaji wenye akili bandia (3)
Washiriki wakijaribu mfumo wa 5G+ wa uendeshaji wa gari bila ya dereva kwenye banda la Kundi la Makaa ya Mawe la Shaanxi la maonyesho ya sita ya kimataifa ya njia ya hariri Tarehe 16, Agosti. (Picha/Xinhua) |
Maonyesho ya 6 ya kimataifa ya Njia ya Hariri yalifunguliwa hivi karibuni huko Xi’an, Mkoa wa Shaanxi wa China. Wageni na wafanyabiashara waliotoka nchi na maeneo zaidi ya 70 ikiwemo Korea Kusini, Thailand, Singapore, pamoja na wafanyabiashara kutoka mikoa zaidi ya 20 humu China walishiriki kwenye maonyesho kwa kupitia video au kwenda kwenye jumba la maonesho.
Katika miaka 9 iliyopita tangu pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” lilipotolewa, thamani ya biashara kati ya China na nchi za “Ukanda Mmoja, Njia Moja” imekuwa ikiongezeka kwa hatua madhubuti. Hivi sasa, viwanda visivyochafua mazingira na utengenezaji bidhaa wa akili bandia vinaendelea kuhimiza maendeleo ya kiwango cha juu ya ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na kuwa ongezeko jipya katika ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kwenye ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma