久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Maduka ya Mitandaoni yanavyobadilisha maisha ya wakulima mkoani Shaanxi, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 08, 2022
Maduka ya Mitandaoni yanavyobadilisha maisha ya wakulima mkoani Shaanxi, China
Msichana ambaye ni maarufu mtandaoni akitangaza moja kwa moja kupitia mtandaoni mazao ya kilimo kwenye Kampuni ya Teknolojia za Biashara ya Kielektroniki ya Shaanxi Huinong huko Wugong, Mji wa Xianyang, Mkoa wa Shaanxi nchini China (Picha na People’s Daily Online)

Matunda, mazao mbalimbali yanauzwa kwa wingi na kuchangia kiuchumi

 Katika miaka minane iliyopita, Serikali ya Mkoa wa Shaanxi nchini China ilitangaza mkakati wa kuvutia biashara za mtandaoni katika eneo la Wugong, Mji wa Xianyang. Lengo kubwa la mkakati huo lilikuwa kuanzisha miradi mingi ya biashara za mtandaoni na kuiunganisha na sekta ya kilimo kwa lengo la kuhimiza biashara ya mazao ya kilimo na kuongeza mapato ya wakulima. Leo hii mikakati hiyo imeleta manufaa makubwa.

Baada ya miaka 8 ya ukuaji na usambazaji kwa kasi wa mazao, Wugong imekuwa msambazaji mkubwa wa chakula na mazao ya kilimo katika eneo la Kaskazini Magharibi mwa China.

Kampuni ya Teknolojia ya Mtandaoni ya Shaanxi Meinong imekuwa ikijihusisha na bidhaa za mauzo ya kilimo kwa miaka 15, na ina vikundi vya wateja wa kuaminika vinavyofikia milioni 40 katika usambazaji wa kijadi.

Kampuni hii ambayo ni injini ya mauzo ya mtandaoni na ya nje ya mtandao ya mazao ya kilimo, imejenga maduka ya kijumuiya yanayojumuisha wakazi zaidi ya milioni 1 katika miji ya Xi'an na miji mingine mikubwa na ya ukubwa wa kati kote nchini China. Thamani ya jumla ya mauzo ya bidhaa zinazohusiana na matunda, chakula, mboga na makundi mengine kwa wateja ilifikia Yuan milioni 850 Mwaka 2021. Katika robo ya kwanza ya Mwaka 2022, mauzo yalikuwa yuan milioni 82.56.

Mwaka 2021, mradi wa ujenzi wa kituo cha usambazaji wa bidhaa za mazao ya kilimo wa Awamu ya Pili wa Shaanxi Meinong ulianza rasmi, ukiwa na uwekezaji wa jumla wa yuan milioni 110. Mradi huu unatarajiwa kukamilika Novemba 2022 na kuanza kutumika. Mradi utakuwa na vifaa vya kusaidia karakana, na utakuwa na karakana za uzalishaji na usindikaji, friji za kuhifadhi bidhaa, majengo ya ofisi, nyumba za wafanyakazi, kantini na kadhalika.

Kampuni hii imejitolea kujenga msingi katika seti ya faida za usindikaji wa bidhaa za kilimo, uhifadhi, mauzo ya mtandaoni, mafunzo ya teknolojia ya biashara za mtandaoni, uoneshaji wa utamaduni wa kibiashara, utangazaji wa biashara ya kielelezo.

Utumiaji wa watu maarufu kutangaza mazao kwenye maduka ya mitandaoni

Kampuni ya Teknolojia za Biashara ya Kielektroniki ya Shaanxi Huinong ina Kituo cha utangazaji wa moja kwa moja wa mazao ya kilimo na bidhaa nyinginezo kwa kutumia watu maarufu wa mtandaoni. Kituo hiki cha Kaskazini-Magharibi kinafadhiliwa na Kituo cha Matunda cha Shaanxi na Serikali ya Eneo la Wugong.

Kampuni hiyo imewekeza zaidi ya Yuan milioni 10 ili kujenga na kuendesha kituo hiki cha matangazo ya moja kwa moja ya biashara ya mtandaoni. Kwa mujibu wa habari kutoka kwenye kampuni hiyo, kituo hiki kina vyumba 30 vya matangazo ya moja kwa moja ya mtandaoni kwa kutumia watu maarufu, watu zaidi ya 70 kutoka kwenye timu ya media, zaidi ya wafanyakazi 20 wa ufundi waliobobea katika utangazaji na usimamizi wa matangazo ya moja kwa moja, na watu maarufu wa mtandao zaidi ya 150 waliosainishwa.

Hadi kufikia sasa makampuni makubwa ya kuendesha biashara za mtandaoni ya China kama vile JD.Com, Kuaishou, Taobao na mengineyo yameingia ubia wa utangazaji wa moja kwa moja na kampuni hii ili kusaidia kuhimiza biashara ya mtandaoni kuwa kubwa na yenye nguvu zaidi.

Tangu kuanzishwa kwake, mauzo ya utoaji bidhaa wa moja kwa moja ya Mwaka 2021 yalifikia zaidi ya yuan bilioni 2, mauzo ya robo ya kwanza ya Mwaka 2022 yalikuwa yuan milioni 620.

Kituo hiki kikiwa na msingi wa matangazo ya moja kwa moja unaolingana na huduma ya wateja, upigaji picha nzuri za bidhaa, sanaa, uendeshaji, ghala na wafanyakazi wengine, kwa kiwango kikubwa zaidi kumerahisisha biashara, na kufanya uuzaji wa bidhaa kuwa jambo rahisi na la kuvutia.

“Tutaunda muundo mpya wa rejareja mtandaoni kupitia huduma za kituo kimoja kama vile matangazo ya moja kwa moja ya kutumia watu maarufu mtandaoni, huduma ya biashara ya mtandaoni, jukwaa la ugavi, utangazaji wa bidhaa, ili kufikia maendeleo ya kunufaishana kati ya wafanyabiashara, wateja na majukwaa ya utangazaji wa moja kwa moja.” Habari kwa vyombo vya babari zilizotolewa na kampuni hiyo zimesema.

Kampuni ya Teknolojia za Mtandao ya Cloud Creative Intelligence

Kampuni hii ni ya biashara ya mtandao inayovuka mipaka ambayo ilianzishwa katika Kaunti ya Wugong Mwezi Juni 2019. Kampuni hii kwa kiasi kikubwa inategemea kampuni Amazon.com, muuzaji mkuu wa bidhaa mtandaoni nchini Marekani.

Habari kutoka kwenye kampuni hii zinaeleza kuwa, kampuni hii imejikita katika bidhaa za viwanda vyepesi vya China kama vile samani ndogo, vifaa vya nyumbani, mavazi, bidhaa zinazotokana na kazi za mikono, na kadhalika.

Na imesaidia sana kwa bidhaa kutoka Shaanxi, hasa eneo la Wugong, kama vile zile za kusukwa kwa mkono, mirija, embroidery, rattan na sifa nyingine za kutengenezwa mikono kusafirishwa kwenda Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Mexico, Canada, Japan, Hispania na nchi na maeneo mengine zaidi ya 30.

Kampuni hii imepanga kuwekeza Yuan milioni 30, katika ujenzi wa mtandao wa wingu wa mauzo ya bidhaa unaotumia akili bandia na kituo cha uchakataji wa data. Mradi huu umegawanyika katika awamu nne za ujenzi, ikiwa ni pamoja na utangazaji wa usajili wa duka, ujenzi wa kituo cha uzalishaji na uleaji vipaji vya kiteknolojia, ujenzi wa sehemu ya kuhifadhi data na miundombinu na ukarabati.

Kwa sasa, ujenzi wa kipindi cha kwanza wa mradi wenye uwekezaji wa yuan milioni 2 umekamilika na kuanza kufanya kazi. Ndani yake kuna maduka 30 na wafanyakazi 30, na wote ni vijana. Baada ya mradi huo kukamilika, utakuwa na maduka 300 na kutoa nafasi za ajira zaidi ya 300. Kiasi cha mauzo ya nje kwa mwaka kitafikia zaidi ya yuan milioni 150.  

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>