Lugha Nyingine
Xi akabidhi nishani ya Agosti Mosi kwa wanajeshi mashuhuri
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping Jumatano wiki hii alikabidhi nishani ya Agosti Mosi kwa wanajeshi watatu na kukabidhi bendera ya heshima kwa kikosi cha kijeshi kwa utumishi wao uliotukuka kabla ya maadhimisho ya miaka 95 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China. (PLA).
Rais Xi, aliwasaidia watu hao kuvaa nishani zao, kuwakabidhi vyeti vya heshima, na kupiga nao picha.
Pia alitunuku bendera ya heshima ya kuheshimu mchango wa kikosi cha mfano cha makombora ya ardhini hadi angani cha Jeshi la Anga la PLA.
Xu Qiliang, Naibu Mwenyekiti wa CMC, alisoma maagizo yaliyotiwa saini na Rais Xi ya kuwapa heshima wanajeshi na kikosi hicho. Hafla ya kukabidhi tuzo hiyo iliyofanyika Beijing, China iliongozwa na Zhang Youxia, ambaye pia ni Naibu Mwenyekiti wa CMC.
Maadhimisho ya miaka 95 tangu kuanzishwa kwa PLA yatafanyika Agosti Mosi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma