Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China akutana na Mwenyekiti Mtendaji wa Baraza la Uchumi Duniani (WEF)
BEIJING - Waziri Mkuu wa China Li Keqiang amekutana na Mwenyekiti Mtendaji wa Baraza la Uchumi la Dunia (WEF) Klaus Schwab kwa njia ya video siku ya Jumanne.
Katika mazungumzo kati yao, Li alisema ushirikiano kati ya China na WEF umepitia safari ya zaidi ya miongo minne, karibu sambamba na mchakato wa mageuzi na kufungua mlango wa China.
Amesema hivi sasa, maendeleo ya Dunia yanakabiliwa na mambo mengi ya kutokuwa na uhakika na yanayoathiri utulivu wake, hata hivyo, amani na maendeleo ya Dunia, na mwingiliano na mawasiliano kati ya nchi ni matakwa ya pamoja ya watu na mwenendo uliopo wa zama hizi.
"Jumuiya ya kimataifa inahitaji kuimarisha kuaminiana, kulinda amani na utulivu, na kukabiliana kwa pamoja na changamoto kwa mazungumzo na mawasiliano ya karibu," Li amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma