Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China asisitiza kuhimiza kwa nguvu mageuzi na kufungua mlango na kuleta utulivu wa nguzo za soko na ajira (3)
FUZHOU - Waziri Mkuu wa China Li Keqiang amehimiza juhudi kubwa za kufanya mageuzi na kufungua mlango, na kuleta utulivu katika maendeleo ya nguzo za soko na ajira.
Li, ambaye pia ni Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, ameyasema hayo alipofanya ziara ya ukaguzi katika Mkoa wa Fujian, Mashariki mwa China kuanzia Alhamisi hadi Ijumaa.
Li alisikiliza ripoti ya kazi ya serikali ya mkoa kuhusu kuleta utulivu wa ajira na kutembelea eneo maalum la uvumbuzi liitwalo Bosssoft. Akisifu mafanikio ya eneo hilo katika kuandaa kulea na kukuza makampuni ya teknolojia ya hali ya juu na kuongeza nafasi nyingi za ajira, Li ameitaka serikali ya mkoa huo kutoa fedha ili kusaidia maeneo ya kuwaandaa wavumbuzi na kupunguza gharama, kama vile kodi.
Akizungumza na wajasiriamali na wahitimu wapya wa vyuo vikuu wanaofanya kazi kwenye eneo hilo, Li amesema China inapaswa kuhimiza ujasiriamali na ubunifu mkubwa kwa kuhamasisha watu wengi zaidi, hasa vijana, kuanzisha biashara na kufanya uvumbuzi.
Alipokuwa akikagua Lioho Machinery, kampuni iliyowekezwa na wafanyabiashara kutoka Taiwan, Li amehimiza kampuni hiyo kupata sehemu kubwa ya soko kupitia uvumbuzi na usimamizi wa ubora.
Li amesikiliza ripoti kuhusu biashara ya nje na uwekezaji katika Mkoa wa Fujian na kukagua bandari ya kimataifa ya nchi kavu ya Jinjiang. Huku akieleza kuwa bandari ni dirisha muhimu la kufungua mlango, na kutoa msaada muhimu kwa uagizaji na uuzaji nje bidhaa, Li amehimiza kuendeleza mageuzi katika kugatua madaraka, kuboresha kanuni, na kurahisisha mazingira ya biashara katika bandari.
Wakati wa ziara yake ANTA Sports, kampuni kubwa ya kibinafsi ya mavazi ya michezo, Li amehimiza kampuni hiyo kushindana katika soko la kiwango cha juu huku ikizingatia kupanua soko la watu wengi na uwezo wake wa kuvutia wanunuzi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma