Lugha Nyingine
Kampuni ya Magari ya BMW yafungua kiwanda kipya nchini China
SHENYANG - Kiwanda kipya cha ubia cha Kampuni ya BMW nchini China kimefunguliwa Alhamisi wiki hii huko Shenyang, Mkoa wa Liaoning, Kaskazini-Mashariki mwa China, kikiwa na uwekezaji wa jumla wa Yuan bilioni 15 (kama dola bilioni 2.2 za Kimarekani).
Kwa mujibu wa taarifa, Kiwanda Lydia cha Kampuni ya magari ya BMW Brilliance (BBA), ambacho ni mradi wa ubia kati ya BMW na kampuni ya Magari ya Brilliance ya China kitaongeza uzalishaji wa magari wa kila mwaka wa BMW nchini China hadi kufikia magari 830,000. BMW imesema ni uwekezaji mkubwa zaidi wa kampuni moja ya kuunda magari ya Ujerumani nchini China.
Kikiwa kimejengwa kwenye Wilaya ya Tiexi ya Shenyang, Kiwanda Lydia cha BMW kinachukua jumla ya eneo la mita za mraba milioni 2.9. Katika kiwanda hicho, kuna majengo mbalimbali kama vile karakana ya kunda bodi la gari, karakana ya kupaka rangi magari, mstari wa uundaji wa mwisho wa sehemu za gari, na kituo kikubwa cha data.
Kiwanda hiki kimeunganishwa na mtandao wa gigabit wa 5G ili kukidhi mahitaji data za intaneti kwa teknolojia kama vile uhalisia uliodhibitishwa (AR) na uwasilishaji wa video kwa wakati halisi.
"Kiwanda Lydia ni cha kwanza ambacho Kampuni ya BMW imepanga na kukamilisha ujenzi wake katika mazingira ya mtandaoni tangu mwanzo wa muundo," amesema Zhang Tao, mkuu wa kiwanda. Ameongeza kuwa, katika hatua ya ujenzi, alikuwa na uwezo wa kuona kwa uhalisia eneo halisi la ujenzi na athari za ujenzi kupitia uhalisia pepe.
Shenyang ni msingi mkubwa wa uzalishaji magari wa Kampuni ya BMW duniani kote. Idadi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo nchini China imezidi 28,000.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma