Lugha Nyingine
Mahali pa Kiwanda cha zamani mjini Xi’an paonekana nguvu mpya ya uhai ya kiuchumi
“Bustani ya teknolojia na uvumbuzi wa utamaduni ya Jihua 3511” iliyoko kwenye eneo la Yanta la Mji wa Xi’an ilikuwa Kiwanda cha 3511 cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA). Kiwanda hicho kilikuwa kiwanda kikubwa zaidi cha kuzalisha taulo nchini China, kikitoa mchangio muhimu kwa ajili ya viwanda vya mahitaji ya kijeshi na uuzaji wa bidhaa nje wa Mkoa wa Shaanxi mwanzoni mwa mageuzi na kufungua mlango.
Hivi sasa, baada ya kufanyiwa usanifu mpya na ukarabati mzuri, sehemu ya kiwanda hicho cha zamani imebadilika kuwa “kituo cha makazi cha aina mpya” kinachohusisha biashara mbalimbali, masoko, maduka, migahawa, samaki wa kuburudisha, maua mazuri na bidhaa zenye uvumbuzi wa kiutamadani. Bustani hiyo inawaletea sehemu ya kustarehesha wakazi wapatao 400,000 walioko karibu nayo, na pia imeonesha nguvu mpya ya uhai ya kiuchumi kwenye sehemu hiyo ya kiwanda cha zamani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma