Lugha Nyingine
Namibia yatarajia kupokea watalii wa kimataifa zaidi ya 500,000 katika Mwaka 2022
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 27, 2022
WINDHOEK - Waziri wa Mazingira wa Namibia, Pohamba Shifeta Alhamisi wiki hii katika taarifa yake amesema kwamba, nchi hiyo inatarajia kupokea watalii wa kimataifa zaidi ya 500,000 katika Mwaka 2022, kutoka watalii 354,508 waliotembelea nchi hiyo Mwaka 2021.
Shifeta amesema janga la UVIKO-19 limeipa Namibia fursa ya kuboresha mfumo wezeshi wa kuanzisha upya sekta hiyo.
“Namibia itazindua programu lengwa za kuingilia kati katika sekta ya utalii kupitia utayarishaji na utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kufufua Utalii wa Mwaka 2022 hadi 2024” amesema.
"Mpango umebainisha sera muhimu, programu za kimkakati na shughuli zinazohitajika ili kurejesha sekta hiyo kuwa na yenye nguvu na bora zaidi," amesema.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma