Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atoa wito wa kuanzishwa kwa njia mpya ya kuendeleza vyuo vikuu vya China viwe vya kiwango cha juu duniani
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping siku ya Jumatatu wiki hii ametoa wito wa kuanzishwa kwa njia mpya ya kujenga vyuo vikuu vya China vya kiwango ha juu duniani.
Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China, ameyasema hayo alipotembelea Chuo Kikuu cha Umma cha China mjini Beijing.
Xi amesisitiza kufuata uongozi wa CPC na kurithisha desturi ya mapinduzi katika kuendesha vyuo vikuu. Pia amesema vyuo vikuu vya China vinapaswa kukita mizizi nchini China na kuepuka kuiga tu vigezo na mifano ya kigeni.
Ziara hiyo imefanyika kabla ya Siku ya Vijana ya China, ambayo hufanyika Mei 4 kila mwaka.
Kwa niaba ya Kamati Kuu ya CPC, Xi ametoa salamu za maadhimisho ya siku hiyo ya vijana wa makabila mbalimbali ya China.
Xi pia ameelezea matumaini yake kwamba vijana wote nchini humu watakumbuka na kuzingatia maagizo ya CPC, kufanya juhudi katika kuleta ustawishaji wa taifa, na kufanya kazi kwa bidii ili kupata matokeo bora zaidi.
Historia ya Chuo Kikuu cha Umma cha China inaweza kufuatiliwa kuanzia Shule ya Umma ya Shanbei, iliyoanzishwa Mwaka 1937. Chuo kikuu hicho kwa miongo kadhaa, kimekuwa kikizingatia ubinadamu na sayansi ya kijamii, na masomo ya Umarx.
Katika ziara yake hiyo, Xi alihudhuria darasa la kisasa linalofundisha kozi za kiitikadi na kisiasa. Amehudhuria darasani na wanafunzi, kusikiliza kwa umakini na kushiriki mijadala.
Alipotembelea Makumbusho ya chuo kikuu hicho, Xi alikutana na maprofesa, wataalam, na wajumbe wa wahadhiri bora vijana na wa makamo na kuzungumza nao.
Xi amesema kujenga vyuo vikuu vya kiwango cha juu duniani kunahitaji wahadhiri wa kiwango cha juu, akisisitiza umuhimu wa kufundisha na kuwaandaa wahadhiri wenye ujuzi.
Xi amesema kuna haja kubwa ya kujibu maswali ya nyakati, kama vile "Ni nini kinatokea kwa Dunia?" na "binadamu wanapaswa kuelekea wapi?"
Katika ziara hiyo Wang Huning na viongozi wengine wakuu wa Serikali Kuu pia wameshiriki.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma