Lugha Nyingine
Shughuli za kukaribisha siku 200 kuelekea Michezo ya 19 ya Asia zafanyika Hangzhou (2)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 23, 2022
Shughuli mbalimbali za kukaribisha siku 200 kuelekea Michezo ya 19 ya Asia zilifanyika huko Hangzhou Jumatatu wiki hii, ambayo ni siku moja baada ya sherehe za ufungaji wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing.
Usiku wa siku hiyo, katika Ziwa Xihu laHangzhou, anga iliangazwa na UAV 1000 hivi. Maonesho ya taa pamoja na maonesho ya upigaji wa muziki yalivutia wakazi wengi kushiriki kwenye shughulihizo.
Miji mitano inayoandaa michezo hiyo kwa pamoja, Ningbo, Wenzhou, Huzhou, Shaoxing, na Jinhua pia ilifanya shughuli mbalimbali za michezo na utamaduni kwa kukaribisha siku 200 kuelekea Michezo ya Asia.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma