Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping ampongeza Malkia Elizabeth II kwa kutimiza miaka 70 ya umalkia
BEIJING - Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za pongezi kwa Malkia Elizabeth II kwa kuadhimisha miaka 70 tangu kutawazwa kuwa Malkia wa Uingereza.
Katika ujumbe huo wa Jana Jumapili, Rais Xi amesema Malkia Elizabeth II kwa muda mrefu amekuwa akijali na kuunga mkono urafiki kati ya Uingereza na China, na ni shuhuda na mhimizaji wa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Akibainisha kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Uingereza katika ngazi ya balozi, Xi ameeleza matumaini yake kwamba pande hizo mbili zitachukua fursa hii kuimarisha urafiki na hali ya kuaminiana, kupanua mawasiliano na ushirikiano, na kufanya kazi kwa pamoja ili kukuza mshikamano wa kimataifa. .
Ameongeza kuwa, Kwa kufanya hivyo nchi hizo mbili zinaweza kuleta manufaa kwa watu wa pande zote, na kutoa mchango mpya katika kusaidia jumuiya ya kimataifa kukabiliana na changamoto mbalimbali na kukuza amani, utulivu, ustawi na maendeleo duniani kote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma