Lugha Nyingine
Xi atembelea Shanxi kabla ya Mwaka Mpya wa China
Rais wa China Xi Jinping, Jumatano alianza ziara yake katika Mkoa wa Shanxi Kaskazini mwa China kabla ya Sikukuu ya Spring, au Mwaka Mpya wa China.
Katika vijiji viwili, Xi alitembelea nyumba za wanavijiji na kukagua ujenzi baada ya maafa katika maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko mwaka jana. Pia alikagua kazi ya wenyeji katika kurejesha kilimo, kuhakikisha upatikanaji wa mfumo wa joto kwa wananchi wakati wa baridi, kuunganisha na kupanua mafanikio ya kupambana na umaskini na kuendeleza maisha ya vijijini.
Kwa miaka 10 mfululizo, Xi akiwa Kiongozi Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amekuwa na desturi ya kuwatembelea watu wa ngazi ya chini, hasa wale wasiojiweza, kabla ya sikukuu ya mwaka mpya wa jadi, sikukuu muhimu zaidi katika kalenda ya China na ni tukio la kukutanisha familia pamoja. Sikukuu ya Mwaka Mpya wa jadi wa China itaanza Tarehe 1 Februari mwaka huu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma