Lugha Nyingine
Rais Xi ahimiza uhusiano mzuri na thabiti kati ya China na Marekani
Rais wa China Xi Jinping ametoa mwito wa kuendeleza uhusiano mzuri na thabiti kati ya China na Marekani.
Akizungumza Jumanne hii kwenye mkutano kwa njia ya video na Rais wa Marekani Joe Biden, Xi amesema China na Marekani zinapaswa kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani, kutafuta ushirikiano wa kunufaishana kwa pande zote, na kusimamia mambo ya ndani vizuri huku zikibeba majukumu ya kimataifa.
Xi amesema kuwa, China na Marekani ziko katika hatua muhimu za maendeleo, na "Kijiji cha Dunia" cha binadamu kinakabiliwa na changamoto nyingi.
Xi amesema China na Marekani, zikiwa nchi zenye uchumi mkubwa zaidi duniani na wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, zinatakiwa kuongeza mawasiliano na ushirikiano, kila upande unapaswa kushughulikia vizuri mambo yake ya ndani huku ikibeba majukumu yake ya kimataifa na kufanya kazi kwa pamoja kuendeleza masuala ya amani na maendeleo duniani.
Amesema, haya ni matumaini ya pamoja ya watu wa nchi hizo mbili na duniani kote, pia ni kazi maalumu za pamoja kwa viongozi wa China na Marekani,
Xi amesisitiza kuwa uhusiano mzuri na thabiti kati ya China na Marekani unahitajika kwa ajili ya kuendeleza maendeleo ya nchi hizo mbili na kulinda hali ya kimataifa yenye amani na utulivu, ikiwa ni pamoja na kutafuta utatuzi wenye ufanisi kwa changamoto za kimataifa kama vile mabadiliko ya tabianchi na janga la UVIKO-19.
China na Marekani zinapaswa kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani, na kutafuta ushirikiano wa kunufaishana, Xi amesema, huku akielezea utayari wake wa kufanya kazi na Rais Biden kujenga maelewano na kuchukua hatua madhubuti za kuusogeza mbele katika mwelekeo chanya uhusiano kati ya China na Marekani.
Xi ameongeza kuwa, kufanya hivyo kutasaidia kuongeza maslahi ya watu wa pande mbili na kukidhi matarajio ya jumuiya ya kimataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma