Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping wa China asisitiza uhusiano imara na Ujerumani, EU katika Mazungumzo kwa njia ya Video na Chansela wa Ujerumani
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amekutana kwa njia ya video na Chansela wa Ujerumani Angela Merkel ambapo wamezungumzia maendeleo ya uhusiano kati ya China na Ujerumani na kati ya China na Umoja wa Ulaya katika miaka ya hivi karibuni na kubadilishana maoni ya kina juu ya masuala husika.
Akipongeza mchango wa Merkel katika kukuza uhusiano kati ya China na Ujerumani na kati ya China na Umoja wa Ulaya akiwa madarakani, Xi amesema kuwa "jambo la maana zaidi la urafiki ni kuelewana, na jambo la msingi la kuelewana kwa watu ni kujua ni nini kiko ndani ya fikra ya kila mmoja”
"Msemo huu siyo tu ni mfano mzuri wa mabadilishano yetu ya kina kwa miaka mingi, lakini pia unaonesha uzoefu muhimu katika kudumisha maendeleo mazuri na uhusiano mzuri kati ya China na Ujerumani kwa miaka 16 iliyopita," Xi ameongeza.
Huku akibainisha kwamba Mwaka 2022 China na Ujerumani zitaadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, Xi amesema kuwa kuendeleza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kwenye njia sahihi ni muhimu sana.
"China daima huchukua uhusiano wake na Ujerumani kwa kupitia mtazamo wa kimkakati na wa muda mrefu, na iko tayari kudumisha mawasiliano ya ngazi ya juu na Ujerumani, kukuza maelewano na urafiki kati ya watu wa pande mbili, kupanua uwezekano wa ushirikiano katika nyanja za jadi, huku tukitafuta maeneo mapya ya ushirikiano katika mageuzi ya nishati na uchumi usioleta uchafuzi na uchumi wa kidijitali, na kuendeleza zaidi uhusiano wa nchi mbili, "Xi amesema.
Kwa upande wake, Merkel amesema anakumbuka mawasiliano yote aliyokuwa nayo na Xi kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita, na kwamba kwa kipindi chote wamekuwa na mazungumzo ya wazi na ya kina juu ya masuala yanayofuatiliwa kwa pamoja, ambayo yameongeza uelewa wa pamoja na kukuza maendeleo mazuri ya uhusiano kati ya Ujerumani na China na kati ya Umoja wa Ulaya na China.
Wakati aliposhika madaraka ya Chansela wa Ujerumani, China imepata maendeleo ya haraka na imeonesha nguvu wake kubwa wa taifa, Merkel amesema, akiongeza kuwa anaamini Umoja wa Ulaya unapaswa kuendeleza uhusiano wake na China kwa uhuru.
"Ninaamini kuwa uhusiano wa Umoja wa Ulaya na China unaweza kuzikabiliwa changamoto mbalimbali na kuendelea kukua," amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma