Mtafiti katika Taasisi ya Elimu ya Sera katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa nchini Ethiopia, Balew Demissie amesema, ushirikiano kati ya China na Afrika umeshinda majaribu ya muda katika mazingira ya kimataifa yanayobadilika na kuzidi kusonga mbele. Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la China Xinhua siku chache kabla ya Mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika wiki hii hapa Beijing, Mtafiti huyo amesema urafiki kati ya pande hizo mbili umeshuhudia mabadiliko mengi ya kihistoria pamoja na changamoto mbalimbali.
Waziri wa Nishati na Petroli wa Sudan Dkt. Mohieddin Naeem Mohamed Saeed amesema, ukweli umethibitisha kuwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) limehimiza utekelezaji wa miradi mingi muhimu ya miundombinu barani Afrika.
(Picha inatoka CRI) Mkutano wa Mwaka 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utafanyika mjini Beijing, China kuanzia Septemba 4 hadi 6. Mtaalamu wa uchumi wa zamani katika Benki ya Dunia ambaye pia ni mshauri wa serikali ya Kenya Dkt.
(Picha inatoka CRI) Mkutano wa Viongozi wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) wa mwaka 2024 ambao ni muhimu kwa uhusiano kati ya pande hizo mbili, utafanyika kuanzia Septemba 4 hadi 6 nchini China. Akizungumzia baraza hilo, Msomi wa Somalia Bw.