Lugha Nyingine
Rais Xi asisitiza kusukuma mbele ufunguaji mlango wa kiwango cha juu ili kuhimiza mageuzi na maendeleo
TIANJIN - Rais wa China Xi Jinping amehimiza maeneo ya kitaifa ya maendeleo ya kiuchumi na kiteknolojia kuchochea hatua kwa hatua nguvu na uwezo wao yenyewe katika kufanya uvumbuzi na kuinua kiwango cha ufunguaji mlango ili kuhimiza kazi ya kuendeleza kwa kina mageuzi na maendeleo ya sifa bora.
Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ameyasema hayo kwenye maagizo yake ya hivi karibuni kuhusu kazi ya maeneo hayo maalum ya maendeleo.
Kujenga maeneo ya kitaifa ya maendeleo ya kiuchumi na kiteknolojia ni hatua muhimu ya China kwa kusukuma mbele mageuzi na ufunguaji mlango, Rais Xi amesema.
Ameyatia moyo maeneo hayo ya maendeleo kuwa watangulizi katika mageuzi na ufunguaji mlango, na kuyahimiza kukamilisha zaidi mifumo ya ufunguaji mlango wa kiwango cha juu.
Rais Xi amesema, maeneo hayo yanapaswa kufanya juhudi za kushiriki katika ujenzi wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, kupanua ushirikiano wa kimataifa na kuvumbua njia za kuvutia uwekezaji.
Pia ameyataka maeneo hayo ya maendeleo kukuza viwanda vya teknolojia za hali ya juu, vya kijani na vya kidijitali, na kuendeleza nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora kulingana na hali halisi ya sehemu yalipo.
Kongamano la kuadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwa kundi la kwanza la China la maeneo ya kitaifa ya maendeleo ya kiuchumi na kiteknolojia limefanyika Tianjin jana Jumapili. Naibu Waziri Mkuu wa China He Lifeng, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, aliwasilisha maagizo hayo ya Rais Xi kwenye kongamano hilo na kutoa hotuba.
Ni muhimu kusoma na kutekeleza maagizo hayo ya Xi, He amesema, akitoa wito kwa maeneo hayo ya kitaifa ya maendeleo ya kiuchumi na kiteknolojia kufanya kazi kwa juhudi za kuhimiza kazi ya kubadilisha muundo wa kiuchumi na kupanda ngazi ya juu.
Naibu Waziri Mkuu wa China, He Lifeng, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akiwasilisha maagizo ya Rais Xi Jinping wa China, na kutoa hotuba kwenye kongamano la kuadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwa kundi la kwanza la China la maeneo ya kitaifa ya maendeleo ya kiuchumi na kiteknolojia lililofanyika Tianjin Kaskazini mwa China, Oktoba 20, 2024. (Xinhua/Zhao Zishuo)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma