久热sm精品视频,亚洲性爱无码免费视频,av无码观看网站重口,久热国产vs视频在线观看

Msaada kutoka Kampuni ya China waboresha elimu katika mitaa ya mabanda ya Mathare nchini Kenya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 18, 2024

Wanafunzi wakionekana katika picha pamoja na madawati mapya yaliyochangiwa shuleni katika mitaa ya mabanda ya Mathare jijini Nairobi, Kenya, Oktoba 15, 2024. (Xinhua/Li Yahui)

Wanafunzi wakionekana katika picha pamoja na madawati mapya yaliyochangiwa shuleni katika mitaa ya mabanda ya Mathare jijini Nairobi, Kenya, Oktoba 15, 2024. (Xinhua/Li Yahui)

NAIROBI - Licha ya umbo lake dogo, Genevive Akinyi ana ujasiri wa kufaulu darasani, jambo ambalo limemfanya apendwe na walimu wa shule yake iliyoko katikati ya mitaa ya mabanda ya Mathare, Nairobi, mji mkuu wa Kenya.

Akinyi, mwenye umri wa miaka 13 na sasa akiwa anasoma darasa la saba, ni mwanafunzi mkarimu na mcheshi katika Kituo cha Elimu cha Hanka, ambacho kimenufaika na msaada wa madawati, makabati na mbao za kuandikia kwa chaki kutoka kwa Kampuni Hodhi ya Transsion, kampuni ya kiteknolojia ya China inayojulikana kwa chapa zake za simu janja zikiwemo Tecno, Itel na Infinix.

Siku ya Jumanne asubuhi yenye hali joto ya unyevu, furaha yake ilikuwa dhahiri wakati alipotazama moja ya madawati ya kuvutia kwenye darasa lake. Akinyi ameonyesha mapenzi yake kwa sayansi jumuishi, sayansi ya jamii, hisabati na lugha, ambayo yote anatumai yatafungua njia kwa ndoto yake ya udaktari.

"Tunafuraha kwa madawati haya mapya. Yanatufanya tupate utulivu wa mwili wakati wa masomo. Msaada kutoka kwa kampuni ya China umetusaidia, na tunatarajia kufanya vyema katika mitihani yetu ya mwisho," Akinyi amesema.

Kikiwa mita chache kutoka ukingo wa mto, Kituo cha Elimu cha Hanka ni muundo mzuri unaofadhiliwa na Jumuiya ya Huduma za Ujenzi wa Ndoto (DBSA), shirika lisilo la faida lililoanzishwa na vijana wa kujitolea wa China Mwaka 2014.

Kituo hiki kina wanafunzi vijana zaidi ya 400 na ni mojawapo ya vituo 15 vilivyojengwa na DBSA katika mitaa hiyo ya Mathare, ambavyo vyote vimefaidika na programu zinazofadhiliwa na mashirika ya hisani, ikiwa ni pamoja na kampuni za China.

Esther Dodo, mwalimu mkuu katika Kituo cha Elimu cha Hanka, amesisitiza mchango muhimu ambao uungaji mkono huo kutoka DBSA na Kampuni ya Transsion umetoa katika kuboresha maisha ya watoto katika makazi hayo yasiyo rasmi ya Mathare.

"Utoaji wa chakula umewawezesha wanafunzi wetu kuzingatia vyema darasani, wakati msaada wa madawati na makabati umeongeza mtazamo chanya miongoni mwa wanafunzi," Dodo amesema.

Hadi sasa, shule 14, vikiwemo vituo vya kulelea watoto nyakati za mchana na shule za msingi na sekondari katika mitaa ya Mathare, zimepokea zana hizi muhimu za kujifunzia, zikinufaisha wanafunzi 2,409, kampuni hiyo ya Transsion imesema.

Wanafunzi wakifanya kazi za masomo kwenye madawati mapya yaliyochangiwa shuleni katika mitaa ya mabanda ya Mathare jijini Nairobi, Kenya, Oktoba 15, 2024. (Xinhua/Li Yahui)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha

<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>