Lugha Nyingine
China yatangaza hatua mpya za kuleta utulivu wa soko la nyumba
Mkutano na waandishi wa habari kuhusu kuleta utulivu katika sekta ya nyumba ukifanywa na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China mjini Beijing, mji mkuu wa China, Oktoba 17, 2024. (Xinhua/Li Xin)
BEIJING - Maafisa wa Serikali ya China siku ya Alhamisi wametangaza hatua mpya ili kuimarisha dalili za utulivu katika sekta ya nyumba, baada ya sera nyingi zinazounga mkono sekta ya nyumba zilizotolewa mwezi uliopita kuleta "mabadiliko chanya sokoni."
Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Mijini na Vijijini wa China, Ni Hong na maafisa wengine wametangaza mpango mpya na kutathmini ufanisi wa sera zilizotangazwa hapo awali kwenye mkutano na waandishi wa habari, baada ya viongozi wa China kuahidi mwezi uliopita kubadili mwelekeo wa mdororo wa soko la nyuma na kuliimarisha.
Katika sera hizo mpya, serikali ya China itaongeza uungaji mkono kwa miradi ya ukarabati wa nyumba za pembezoni za mijini na zilizochakaa, Ni amesema, akiongeza kuwa China itakarabati nyumba kama hizo zaidi ya milioni 1 kwa hatua kama vile kutoa fidia ya kifedha kwa wakaazi.
Waziri huyo amesisitiza kuwa miradi yote inayostahiki ya nyumba itajumuishwa katika utaratibu wa "orodha nyeupe" na kwamba mahitaji yake ya kifedha yatatimizwa kupitia mikopo.
Chini ya utaratibu wa "orodha nyeupe" uliozinduliwa Januari mwaka huu, mamlaka za serikali za mitaa zinapendekeza kwamba taasisi za mambo ya fedha zitoe uungaji mkono kwa miradi inayostahiki ya nyumba.
Hadi kufikia Oktoba 16, mikopo iliyoidhinishwa kwa ajili ya miradi ya nyumba ya "orodha nyeupe" ilikuwa imefikia yuan trilioni 2.23 (dola za Marekani kama bilioni 313), Xiao Yuanqi, naibu mkuu wa Idara ya Taifa wa Udhibiti wa Fedha ya China, amesema katika mkutano huo na waandishi wa habari.
Picha hii iliyopigwa tarehe 15 Machi 2024 ikionyesha eneo la ujenzi wa nyumba za makazi chini ya mradi wa ukarabati wa miji katika Wilaya ya Jing'an, mjini Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua/Fang Zhe)
Picha hii ikionyesha watu wakitazama mfano wa mradi wa nyumba mjini Shanghai, Mashariki mwa China, Mei 28, 2024. (Xinhua/Zheng Juntian)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma