Lugha Nyingine
Ripoti yaonesha watu?milioni 8 katika miji mikubwa ya China wanasafiri kwa usafiri wa umma wa mijini kilomita zaidi ya 50 kila siku
Picha iliyopigwa kwa simu ya mkononi ikionyesha watu wakiwa wamepanda eskaleta kwenye stesheni ya sabwei mjini Beijing, mji mkuu wa China, Mei 11, 2021. (Xinhua/Ju Huanzong)
BEIJING - Katika miji 22 ya China yenye watu wengi zaidi, watu wanaotumia usafiri wa umma wa mijini kwa masafa marefu bado wanakabiliwa na changamoto, huku watu zaidi ya milioni 8 wakisafiri kilomita zaidi ya 50 kila siku, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa jana Alhamisi na taasisi ya utafiti chini ya Wizara ya Nyumba na Maendeleo ya Mijini na Vijijini ya China, kwa ushirikiano na Taasisi ya Mipango na Usanifu Miji ya China.
Ikifuatilia miji mikubwa 45 ya China yenye usafiri wa umma wa mijini wa reli, ripoti hiyo inaonyesha kuwa kati ya miji 22 yenye wakazi zaidi ya milioni 5, Beijing ina idadi kubwa zaidi ya watu wanaotumia usafiri huo wa umma wa mijini kwa umbali mrefu, ikiwa na asilimia 12 wanaosafiri zaidi ya kilomita 50, ikifuatiwa na Guangzhou kwa asilimia 10.
Kwa upande wa safari hizo kwa njia moja, asilimia 28 ya watu wanasafiri kwa dakika zaidi ya 60 katika mji mkuu huo wa China, huku Shanghai, Chongqing, Tianjin, Wuhan na Qingdao, asilimia zaidi ya 15 ya watu wakianguka katika kundi hilo.
Mmoja wa watu wnaotumia usafiri wa umma wa mijini kwa umbali mrefu mwenye jina la ukoo la Sun ana umri wa miaka 46. Kila siku ya wiki, anaondoka nyumbani kwake Tianjin, mji wenye watu milioni 13.6 jirani na Beijing, karibia saa 12 asubuhi, anaendesha gari hadi eneo la maegesho karibu na Stesheni ya Reli ya Tianjin, kisha kuchukua reli ya mwendokasi na baadaye sabwei ili kufika mahali pake pa kazi mjini Beijing - - karibu saa mbili, safari ya kwenda njia moja ambayo amedumisha kwa muongo mmoja.
Kwa watu wengi wanaosafiri kwa umbali mrefu kama Sun katika miji mikubwa, huduma za usafiri wa reli mijini bado zinahitaji uboreshaji.
Guo Jifu, mkurugenzi wa Taasisi ya Usafiri ya Beijing, ameeleza kuwa miji mikubwa yenye sehemu kubwa ya sekta ya uchumi wa huduma inapata changamoto zaidi kusawazisha maeneo ya kazi na makazi.
Kwa mujibu wa Yang Zeng, profesa katika Chuo Kikuu cha Shanghai, mkondo wa kuishi na kufanya kazi katika miji yote nchini China ni wa kipekee na unatofautiana na hali iliyo katika nchi za Magharibi na jambo hili linaonyesha uwezo wa muda mrefu.
Watu wakionekana kwenye Stesheni ya Sabwei ya Hujialou mjini Beijing, mji mkuu wa China, Mei 11, 2021. (Xinhua/Ju Huanzong)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma