Lugha Nyingine
Bodi ya Utalii ya Kenya Yazindua Kampeni ya Kuboresha biashara ya Utalii
Bodi ya Utalii ya Kenya (KTB) imeanzisha kampeni mpya itakayoweza kuongeza idadi ya watalii wanaofika nchini Kenya, ikitumia balozi na vituo vya Kenya katika nchi za kigeni.
Kampeni hiyo, iitwayo 'Safari ya Kitalii Kenya: Diaspora Mmoja, Mtalii Mmoja,' inalenga Wakenya zaidi ya milioni 3 walio nje ya nchi kuhamasisha utalii kupitia mitandao yao na kuboresha biashara ya utalii nchini Kenya.
Mkurugenzi Mtendaji wa KTB, June Chepkemei, amesema kuwa Kenya ina balozi 66 ambazo zinawakilisha nchi na kwamba miundombinu hii inatoa fursa bora ya kuiweka Kenya kuwa kivutio kikuu kwa watalii wa kimataifa pamoja na kivutio cha wawekezaji wa kibiashara.
Kampeni hiyo inalenga kuongeza idadi ya watalii kutoka milioni 1.9 hadi milioni 5 ifikapo mwaka 2027, hivyo kuimarisha nafasi ya Kenya katika nyanja ya utalii.
Chepkemei amesisitiza kuwa KTB itawapa Wakenya wanaoishi nje ya nchi motisha ili kuhamasisha utalii katika mitandao yao ya kijamii, ikifanya kazi na sekta ya usafiri kuleta mabadiliko hayo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma