Lugha Nyingine
Rais Xi asema China inapenda kushirikiana na Indonesia katika kuhimiza ujenzi wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping kwenye mazungumzo yake kwa njia ya simu na Rais wa Indonesia Joko Widodo siku ya Jumatatu amesema kuwa China inapenda kushirikiana na Indonesia katika kuhimiza pamoja ujenzi wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, kuhakikisha uendeshaji endelevu wa Reli ya Mwendokasi ya Jakarta-Bandung, na kuanzisha mambo muhimu zaidi ya ushirikiano ili kuleta manufaa mazuri zaidi kwa watu wa nchi zote mbili.
Rais Xi amesema, katika muda wake wa miaka 10 wa kushika madaraka ya Rais wa Indonesia, Widodo ameitembelea China mara nane na kukutana na Rais Xi mara 12, jambo ambalo lilipelekea nchi hizo mbili kufungua ukurasa mpya wa kujenga kwa pamoja jumuiya yenye mustakabali wa pamoja, vilevile kujenga muundo mpya wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote.
Xi amesema, China inathamini sana mchango muhimu aliotoa Widodo kwa ajili ya urafiki wa China na Indonesia, China inaamini kuwa serikali mpya ya Indonesia itaendelea kufuata sera yake ya urafiki kwa China na kusukuma ujenzi wa jumuiya ya China na Indonesia yenye mustakabali wa pamoja kwenye ngazi ya juu.
Rais Xi akieleza kuwa mwaka ujao ni maadhimisho ya miaka 70 tangu kufanyika Mkutano wa Bandung, upande wa China unapenda kushirikiana na Indonesia katika kuenzi Kanuni Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani na Moyo wa Bandung, kuimarisha mshikamano na ushirikiano kati ya nchi za Kusini mwa Dunia, kulinda maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea, na kuhimiza maendeleo, ustawi na utulivu wa kikanda na dunia nzima.
Kwa upande wake, Rais Widodo amesema, katika muongo mmoja uliopita, amejenga urafiki mkubwa na Rais Xi, ambapo mafanikio makubwa yamepatikana katika uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote na ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali.
Ametoa shukurani kwa China kwa kuchangia maendeleo ya kiuchumi ya Indonesia, akisema kuwa Reli ya mwendokasi ya Jakarta-Bandung imekuwa mfano wa kuigwa kwa ujenzi wa pamoja wa Ukanda Mmoja, Njia Moja kati ya pande hizo mbili.
Widodo pia ameeleza imani kuwa chini ya uongozi wa serikali mpya ya Indonesia, uhusiano wa Indonesia na China utadumisha mwelekeo wa ukuaji wa kasi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma