Lugha Nyingine
Rais wa China atoa salamu za pongezi kwa rais mpya wa Ethiopia
Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za pongezi kwa Bw. Taye Atske-Selassie Amde kwa kuchaguliwa kuwa rais mpya wa Ethiopia.
Rais Xi amesema, katika miaka ya hivi karibuni uhusiano kati ya China na Ethiopia umeshuhudia maendeleo ya kasi na ya pande zote, huku kukiwa na kuaminiana kisiasa na manufaa yenye matunda katika ushirikiano wa matokeo halisi kwenye nyanja mbalimbali.
Rais Xi amesema anaweka umuhimu mkubwa kwenye maendeleo ya uhusiano kati ya China na Ethiopia, na anapenda kushirikiana na Rais Taye kutumia fursa ya kutekeleza matokeo ya mkutano wa kilele wa mwaka 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika kusukuma ushirikiano wa kimkakati wa nyakati zote kati ya China na Ethiopia kwa ajili ya kupata mafanikio mapya na kunufaisha vyema watu wa nchi hizo mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma