Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping atoa salamu kwa wazee katika siku ya kuamkia Siku ya Wazee ya China
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) ametoa salamu kwa wazee katika siku ya kuamkia Siku ya Wazee ya China ya leo tarehe 9 ya mwezi wa 9 kwa kalenda ya kilimo ya China mwaka huu, akielezea matumaini yake kwamba wazee wanaweza kupata utunzaji mzuri, kufurahia maisha yao, na kuendelea na utafutaji wao.
Rais Xi ameyasema hayo katika barua yake kwa wajumbe wa wazee wanaoshiriki katika shughuli za kitaifa za watu wa kujitolea.
Katika barua yake, Rais Xi amesema, wazee washiriki wa shughuli hizo za “Harakati za Wazee Wanaojitolea” wamefanya juhudi za kushiriki kwenye shughuli za kujitolea katika miaka ya hivi karibuni, ambapo wakitumikia umma kwa ujuzi na uwezo wao, na kwa maarifa yao ya kazi walizokuwa wamezoea zaidi.
Hayo yote yameonesha Sura na moyo wa wazee wa China katika zama mpya, Rais Xi amesema.
Amesema kuwa wazee ni mali ya thamani na muhimu kwa Chama na nchi, Rais Xi ametoa wito kwa kamati za Chama na serikali katika ngazi zote kutoa kipaumbele kwa kazi zinazohusu wazee.
Idadi ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 60 nchini China ilikuwa imekaribia milioni 300 hadi kufikia mwisho wa Mwaka 2023. Inakadiriwa kuwa itazidi milioni 400 ifikapo Mwaka 2035 na kufikia milioni 500 ifikapo Mwaka 2050.
Rais Xi amehimiza jitihada za kujikita katika kushughulikia matatizo ya wazee, kukamilisha sera na hatua husika, kujenga mazingira mazuri ya kijamii, kuhakikisha ustawi na haki zao vinalindwa, na kuwawezesha kuchangia ipasavyo kwa jamii.
Shughuli hizo zilianzishwa Mwaka 2003 kwa lengo la kutumia utaalamu na ujuzi wa wataalamu wazee katika sekta mbalimbali ili kusaidia katika maendeleo ya maeneo ambayo hayajaendelea vizuri.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma