Lugha Nyingine
Kenya kuandaa kongamano la kuendeleza?shughuli za biashara zinazozingatia haki za binadamu barani Afrika
Kongamano la tatu la Biashara na Haki za Kibinadamu barani Afrika limefunguliwa Jumatano mjini Nairobi nchini Kenya, huku wajumbe wakitoa wito wa kufungamanishwa kanuni za usawa, haki na ujumuishaji katika sekta binafsi barani humo.
Kongamano hilo la siku mbili, lililoitishwa na muungano wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na jumuiya za kikanda, linafanyika chini ya kaulimbiu "Kuhimiza uwajibikaji wa biashara katika dunia inayobadilika kwa kasi."
Washiriki zaidi ya 500, wakiwemo watunga sera, wasimamizi wa sekta, wanadiplomasia, wawakilishi wa wasomi na asasi za kiraia, wanahudhuria kongamano hilo ambalo linalenga kuhimiza mazungumzo na kujifunza kwa kutumia mifano ya biashara inayoendeleza shughuli endelevu na za kimaadili.
Mwanasheria Mkuu wa Kenya Dorcas Oduor amesema Bara la Afrika linazidi kutambua uhusiano muhimu kati ya shughuli za biashara na ulinzi wa haki za binadamu, akisisitiza kuwa Kenya ni nchi ya kwanza ya Afrika kuandaa mpango wa utekelezaji wa kitaifa kuhusu biashara na haki za binadamu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma