Lugha Nyingine
Mkutano wa Mawasiliano ya Vipaji wa Asia Kaskazini-Mashariki (Shenyang) Mwaka 2024 kufanyika Tarehe 24, Oktoba mjini Shenyang
Wang Zhigang, Katibu wa Kikundi cha Uongozi wa Chama ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu na Hifadhi ya Jamii ya Mji wa Shenyang, Mkoa wa Lianoing, China akitangaza masharti hitajika ya nafasi za ajira kwenye mkutano huo. (Picha na Ren Fengtao/People’s Daily Online)
Mkutano wa Mawasiliano ya Vipaji wa Asia Kaskazini-Mashariki (Shenyang) Mwaka 2024 na Mkutano wa Uendelezaji wa Kampuni Adimu za Thamani za China zenye Uwezekano utafanyika kwenye Mji wa Shenyang, Mkoa wa Liaoning, China Oktoba 24, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika hivi karibuni kwenye Jengo la People’s Daily Online.
Wang Zhigang, Katibu wa Kikundi cha Uongozi wa Chama ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu na Hifadhi ya Jamii ya mji huo wa Shenyang, amesema kuwa, hadi sasa mkutano huo wa awamu ya kwanza umeshakusanya taarifa 76,000 za uajiri wa wafanyakazi kutoka kampuni 2,357 katika eneo la Kaskazini-Mashariki, na inatarajiwa kufikia nafasi 100,000 kabla ya mkutano huo kuanza.
Amesema, miongoni mwa nafasi hizo za ajira, kuna nafasi 1,321 za ajira zenye umaalum wa nguvu mpya za uzalishaji kama vile algoriti za udhibiti wa upangaji, wahandisi wa usanifu wa miundo, wahandisi wa usanifu wa uoni wa macho, n.k..
Amesema, kampuni mbalimbali za teknolojia ya hali ya juu za Shenyang hutoa fursa za kazi zaidi ya 1,000.
Mji wa Shenyang pia umeanzisha sera ya ruzuku kwa vipaji na kwamba huwapatia watu wa vipaji vya ngazi za ABC motisha inayoanzia yuan 500,000 hadi yuan milioni 1, fedha za miradi ya utafiti wa kisayansi kuanzia yuan 700,000 hadi yuan milioni 5, na kutoa ruzuku mahsusi kwa "mradi + timu" inayoongozwa na wanasayansi wa kimkakati ambao wanatoa mchango muhimu katika maendeleo ya nyanja.
Kwenye mkutano huo, Mji wa Shenyang pia utazindua“Kituo cha Vipaji cha Asia Kaskazini-Mashariki (Shenyang)" ili kuzidisha zaidi ushirikiano jumuishi wa kikanda wa vipaji.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma