Lugha Nyingine
China yatoa wito kwa pande zote kufanya juhudi za?pamoja kudumisha amani, utulivu kwenye Peninsula ya Korea
BEIJING - Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Mao Ning ametoa wito siku ya Jumatano kwa pande zote kufanya juhudi za pamoja ili kudumisha amani na utulivu kwenye Peninsula ya Korea na kuendeleza mchakato wa suluhu ya kisiasa ya suala la Peninsula ya Korea.
Habari zinasema kuwa Korea Kaskazini (DPRK) imesema itafunga kabisa barabara na reli zinazounganishwa na Korea Kusini (ROK) na kujenga ngome katika maeneo husika ya upande wake kwa miundo imara ya ulinzi kuanzia jana siku ya Jumatano. Habari zinasema kuwa DPRK itachukua hatua kubwa ya kijeshi kutenganisha kabisa eneo la DPRK, ambalo liko ndani ya mamlaka yake, na eneo la Korea Kusini.
Katika kujibu swali linalohusiana na hilo, Msemaji Mao amesema katika mkutano na wanahabari Jumatano kwamba China inafuatilia maendeleo ya hali kwenye Peninsula ya Korea na uhusiano kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini.
"China inaamini kwamba kudumisha amani na utulivu kwenye Peninsula ya Korea na kuendeleza mchakato wa suluhu ya kisiasa ya suala la Peninsula ya Korea kunatumikia maslahi ya pamoja ya pande zote, na ndivyo jumuiya ya kimataifa inatarajia," Mao amesema, akiongeza pande zote zinapaswa kufanya juhudi za pamoja kwa lengo hilo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma