Lugha Nyingine
China inaunga mkono kithabiti ujenzi wa Jumuiya ya ASEAN - Waziri Mkuu wa China
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Wattay mjini Vientiane, Laos, Oktoba 9, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)
VIENTIANE - China inaunga mkono kithabiti ujenzi wa Jumuiya ya Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN), na vile vile nafasi kuu ya ASEAN katika ushirikiano wa kikanda na mchango wake mkubwa zaidi katika mambo ya kimataifa, Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema katika taarifa yake ya maandishi alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Wattay mjini Vientiane jioni ya Jumatano.
Waziri Mkuu Li amewasili nchini humo ambapo atahudhuria mikutano ya viongozi kuhusu ushirikiano wa Asia Mashariki, na kufanya ziara rasmi nchini Laos kutokana na mwaliko wa Waziri Mkuu Sonexay Siphandone, ambaye ni mwenyekiti wa sasa wa ASEAN.
Katika taarifa hiyo, Waziri Mkuu Li ameeleza kuwa China ingependa kufanya mazungumzo ya kina na ya pande zote kuhusu masuala makuu ya ushirikiano wa kikanda na kutoa juhudi za pamoja ili kulifanya eneo hilo liwe injini muhimu kwa maendeleo ya kimataifa.
Katika taarifa hiyo, Li amesema kuwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu, Laos imekuwa na wajibu mkubwa kama mwenyekiti wa zamu wa ASEAN, ikijikita katika ushirikiano wenye matokeo halisi, kujenga maelewano kati ya pande zote, na kuhimiza ujenzi wa Jumuiya ya ASEAN na ushirikiano wa Asia Mashariki kupata maendeleo na mafanikio mapya.
Li amesema kuwa katika miaka ya hivi karibuni, chini ya mwongozo wa kimkakati wa Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), na Rais Thongloun Sisoulith wa Laos ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi, China na Laos zimeendelea kuzidisha na kuimarisha ushirikiano wao wa kimkakati wa pande zote, na uhusiano kati ya pande mbili umeingia katika zama mpya ya kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja.
Akiwa nchini humo, Waziri Mkuu Li atahudhuria Mkutano wa Kilele wa 27 wa China na ASEAN, Mkutano wa Kilele wa 27 wa ASEAN + 3 na Mkutano wa Kilele wa 19 wa Asia Mashariki utakaofanyika kuanzia Oktoba 9 hadi 12.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Wattay mjini Vientiane, Laos, Oktoba 9, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma