Lugha Nyingine
Uganda yaipongeza China kuwa mshirika wa kimkakati katika kuongeza kasi ya maendeleo
Makamu wa Rais wa Uganda Jessica Alupo amesema China ni mshirika wa kimkakati katika kuiunga mkono Uganda kuongeza kasi yake ya maendeleo.
Bi. Alupo amesema hayo katika hafla iliyoandaliwa siku ya Jumatano wiki hii na Ubalozi wa China nchini Uganda mjini Kampala kuadhimisha miaka 75 ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China.
Makamu huyo wa rais amesema licha ya ufadhili wa China uliotangazwa katika mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika hivi karibuni mjini Beijing, Uganda pia imesaini makubaliano ya ushirikiano na China ili kuimarisha biashara ya pande mbili.
Akizungumza katika hafla hiyo, Balozi wa China nchini Uganda Zhang Lizhong amesema, wakati wa mkutano wa kilele wa FOCAC, China na Uganda zilithibitisha uamuzi wao wa kuinua uhusiano wao kuwa ushirikiano wa washirika wa mkakati wa pande zote unaojikita katika maafikiano ya pamoja.
Amesema katika miaka iliyopita, China imekuwa mshirika muhimu wa Uganda, hususan katika kuendeleza sekta za miundombinu ya usafiri na nishati nchini humo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma