Lugha Nyingine
China yawa moja ya nchi inayopanda kwa kasi zaidi kwenye orodha ya nchi zenye uchumi vumbuzi duniani
(CRI Online) Septemba 27, 2024
Ripoti ya “Faharisi ya Uvumbuzi Duniani (GII) Mwaka 2024” iliyotolewa jana Alhamisi na Shirika la Haki Miliki Duniani(WIPO) inaonesha kuwa, China imepanda kwa nafasi moja zaidi katika orodha ya nchi zenye uchumi vumbuzi dunini kwa kusogea nafasi ya 11 duniani, ikiifanya kuwa moja ya nchi iliyopanda kwa kasi zaidi kwenye orodha hiyo katika kipindi cha muongo uliopita.
Ripoti hiyo pia imeonesha kuwa, China inaendelea kuwa nchi pekee ya uchumi wa kipato cha kati kuwa kwenye kundi la nchi 30 za juu kwenye orodha hiyo ya uvumbuzi duniani.
China inashika nafasi ya kwanza katika vipengele vinane vya faharisi za uvumbuzi kati ya 78.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma