Lugha Nyingine
Waziri wa Mambo ya Nje wa China ahudhuria Mazungumzo ya 8 ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa China na nchi za Jumuiya ya CELAC
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akihudhuria Mazungumzo ya Nane ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa China na Nchi za Jumuiya ya Latini Amerika na Karibiani (CELAC) kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York, Septemba 24, 2024. (Xinhua/Xie E)
UMOJA WA MATAIFA - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi Jumanne alihudhuria Mazungumzo ya Nane ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa China na Nchi za Jumuiya ya Latini Amerika na Karibiani (CELAC) kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York akisema kuwa nchi za Latini Amerika na Karibiani ni sehemu muhimu ya "Nchi za Kusini," na vilevile washiriki wenye juhudi na wachangiaji katika usimamizi wa Dunia.
Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amesisitiza kuwa China itaendelea kufuata kanuni ya kutafuta mambo mazuri makubwa zaidi na maslahi ya pamoja, kuimarisha mshikamano na ushirikiano na nchi za Latini Amerika na Karibiani, kutekeleza “mapendekezo matatu makubwa”, kuhimiza uoanishaji kati ya ujenzi wa pamoja wa sifa bora wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na mikakati ya maendeleo ya nchi za eneo hilo, na kuendeleza kwa kina na kuongeza mambo katika ujenzi wa jumuiya ya China na Latini Amerikai na Karibiani yenye mustakabali wa pamoja, ili kuleta manufaa zaidi kwa watu wa pande zote mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma