Lugha Nyingine
Meli ya matibabu ya jeshi la majini la China yamaliza ziara yake nchini Jamhuri ya Kongo na kuelekea Gabon
(CRI Online) Septemba 23, 2024
Meli ya matibabu ya Jeshi la Majini la China "Peace Ark" imekamilisha kwa mafanikio ziara nyingine nchini Jamhuri ya Kongo na kuondoka Bandari ya Pointe-Noire nchini humo kuelekea Gabon, nchi ambayo itakuwa ni kituo cha nane cha ujumbe huo.
Katika ziara hiyo ya siku saba, meli hiyo imetibu jumla ya watu 4,450, kufanya uchunguzi kwa ziada zaidi ya watu 2,300, na kufanikiwa kufanya upasuaji kwa watu 127.
Aidha, meli hiyo pia ilituma timu za wataalam kwa hospitali za mitaa kufanya matibabu ya pamoja ili kuimarisha mabadilishano ya pande zote na kuongeza kuaminiana kati ya pande hizo mbili.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma