<sup id="ggg8g"><ul id="ggg8g"></ul></sup>
<noscript id="ggg8g"></noscript>
  • <nav id="ggg8g"><code id="ggg8g"></code></nav>
  • <sup id="ggg8g"><delect id="ggg8g"></delect></sup>
  • <small id="ggg8g"><menu id="ggg8g"></menu></small>

    久久精品蜜芽国产亚洲av,国产成人观看免费全部完,1024综综合合久久AV,午夜国产成人精品,国产精品综合承认,国产高跟黑色丝袜在线

    Wito wa kimataifa watolewa kwa kuoanisha sera kuhusu kuhamia kwenye nishati safi

    (Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 23, 2024

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu tabianchi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Juni 15, 2023. (Xinhua/Xie E)

    NEW YORK - Katika siku ya kuamkia Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Siku za Baadaye, wataalam na wanadiplomasia walikusanyika kwenye mkutano wa ngazi ya juu katika Chuo Kikuu cha Columbia nchini Marekani siku ya Jumamosi, wakitoa wito wa kuhamia kwenye nishati mpya kwa haraka, kuimarisha uvumbuzi na ufadhili bora ili kuwezesha maendeleo ya nishati safi duniani ambayo yatafaidisha watu na mataifa zaidi.

    Wamesema, kuhamia kwenda kwenye nishati safi ndiyo njia pekee ya kuondoa janga la tabianchi na kufikia maendeleo endelevu, na miaka 10 ijayo itakuwa kipindi cha mafanikio ya mageuzi hayo katika ngazi ya kimataifa, huku wakisema, lazima nchi zijitahidi kuzuia utoaji wa hewa ya kaboni na kuelekea kwenye upunguzaji mkubwa ifikapo Mwaka 2035.

    Kuhamia kwenye Nishati Safi

    Kuna matatizo mengi ya kushughulikiwa, kwani uhaba wa utoaji wa umeme bado unanyima watu zaidi ya milioni 600 kupata umeme, kuhamia kwenye nishati mpya bado kupo nyuma sana huku nishati ya kisukuku ikichukua asilimia zaidi ya 80 ya matumizi yote ya nishati duniani, na kujilinda kibiashara na kizuizi cha kiufundi huzuia maendeleo ya tasnia ya nishati mpya, Cheng Zhiqiang, katibu mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Muunganisho na Ushirikiano wa Nishati Duniani (GEIDCO), amesema kwenye mkutano huo pembezoni mwa mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa.

    Mfalme Letsie III wa Lesotho amesema katika hotuba yake kuu, "Lazima tukabiliane na ukweli ana kwa ana," na "kuichukulia nishati mbadala kama msingi wa uchumi wa taifa letu,"

    Watembeleaji wa maonyesho wakifahamishwa kuhusu gari la muundo mpya lilikuwa likionyeshwa kwenye Mkutano wa Dunia wa Viwanda Mwaka 2024 mjini Hefei, Mkoa wa Anhui, mashariki China, Septemba 21, 2024. (Xinhua/Fu Tian)

    Fu Cong, mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa amesema China inaendelea kuwa kinara katika kuhamia kwenda uchumi wa kijani unaotoa kaboni chache, mhimizaji wa ushirikiano wa kimataifa kwa mageuzi hayo, na mchangiaji katika usimamizi wa nishati na tabianchi duniani.

    Magari yanayotumia nishati mpya ambayo tunatengeneza yamekuwa yakipendwa kote duniani, amesema mwanadiplomasia huyo mkuu.

    Azimio la Nishati ya siku za Baadaye

    Azimio la Nishati ya Siku za Baadaye la mkutano huo ambao umetathmini changamoto, mwelekeo na mtazamo wa maendeleo ya nishati ya siku za baadaye na kupendekeza mipango 10 muhimu ya kuhimiza uhamaji wa kwenda nishati mpya duniani limetolewa.

    Azimio hilo linatoa wito kwa "nchi zote kufanya kazi pamoja ili kuharakisha uhamaji wa kwenda mifumo ya nishati ya siku za baadaye na kufikia maendeleo endelevu kwa binadamu wote."

    (Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

    Picha

    久久精品蜜芽国产亚洲av