Lugha Nyingine
Matembezi ya Mji: Kutembea katika Mtaa wa Utamaduni wa Kale wa Tianjin
Mtaa wa Utamaduni wa Kale wa Tianjin, China ambao pia unajulikana kwa jina la "Jinmen Guli", ikimaanisha " Maskani Tianjin", ni mahali pa kwanza pa Tianjin pa shughuli mbalimbali za biashara, na pia ni kituo kimoja kilichoonekana wazi kwa mila na desturi za utamaduni cha mji huo.
Mtaa huu uko katika Eneo la Nankai la Tianjin na una maduka mengi yenye chapa maarufu yaliyoanzishwa zamani sana. Kwa miaka mingi, mtaa huu umepitia hatua mbalimbali kutoka kituo cha mila na desturi hadi sehemu yenye mambo ya kisasa ya utalii na sehemu ya biashara. Ukiwa na njia nne za watembea kwa miguu, mtaa wake mkuu sasa umekuwa mtaa wa uwazi wa biashara kwa watembea kwa miguu, ukiwa na urefu wa mita 687 na ukichukua eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 13,000.
Mtaa huu ulifunguliwa rasmi mwaka 1986, ukiwa na maduka yenye usanifu wa majengo ya Enzi ya Qing ya China ya Kale (1644-1911). Kwa mamia ya miaka, mtaa huu siku zote umekuwa alama ya mji huo.
Maandazi ya Goubuli yaliyopikwa kwa mvuke, desserts tamu na vyakula vingine vitamu vya kienyeji vyote vinaweza kuonjwa hapa. Zaidi ya hayo, watembeleaji wanaweza kununua sanamu za udongo za rangi, vitu vya kale, vitu vya maandiko ya Kichina, tiara, picha za uchoraji za Mwaka Mpya wa Jadi wa Yangliuqing na bidhaa nyingine nyingi maalum hapa, au kupata hali changamani ya ajabu katika karakana.
Kwa bidhaa bora, bei nafuu, na kuwapa watembeleaji vitu vya kibunifu, mtaa huu wa kihistoria pia umevutia wateja kutoka mbali.
Ukiwa ni mtaa wa biashara kwa watembea kwa miguu na sehemu maarufu ya watalii, Mtaa wa Utamaduni wa Kale wa Tianjin unawahudumia watembeleaji wake kwa kujionea “Tianjin yenye hali halisi ya awali ".
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma