Lugha Nyingine
Waziri wa Mambo ya Nje wa China akutana na Mkuu wa Umoja wa Wabunge wa Jamhuri ya Korea na China
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Kim Tae-nyeon, Mkuu wa Umoja wa Wabunge wa Jamhuri ya Korea na China, mjini Beijing, China, Septemba 18 , 2024. (Xinhua/Yue Yuewei)
BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amekutana na ujumbe unaoongozwa na Kim Tae-nyeon, mkuu wa Umoja wa Wabunge wa Jamhuri ya Korea na China, siku ya Jumatano mjini Beijing ambapo amesema kwamba anathamini mchango uliotolewa na umoja huo kwa ajili ya kuendeleza urafiki kati ya nchi hizo mbili.
Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amesema China na Jamhuri ya Korea (ROK) zinapaswa kuwa majirani wema wa kuaminiana na washirika wazuri wanaofanya ushirikiano wa kunufaishana, bila kujali namna hali ya kimataifa au kikanda inavyobadilika.
Wang ameeleza kuwa sera ya China kuhusu Jamhuri ya Korea siku zote ni ile ile, China inatumai upande wa Jamhuri ya Korea utaelekea lengo sawa na upande wa China, kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa na kusukuma mbele maendeleo mazuri na endelevu ulio tulivu ya uhusiano kati ya China na Jamhuri ya Korea.
Wang amesema China ina nia ya kuanzisha na kufuatilia hatua za kurahisisha zaidi mawasiliano kati ya watu wa nchi hizo mbili, na inakaribisha watu wa makundi mbalimbali kutembelea China.
Ameongeza kuwa China inaendelea kuwa tayari kupanua ushirikiano wa kunufaishana na Jamhuri ya Korea, kufanya juhudi za pamoja ili kulinda kanuni za biashara huria, na kudumisha minyororo ya uzalishaji na utoaji bidhaa iliyo imara, na isiyozuiliwa.
Kwa upande wake Kim na wabunge wengine waliohudhuria mkutano wamesema umoja huo unapenda kushikana mikono na upande wa China ili kuimarisha mawasiliano ya kimkakati, kuongeza mawasiliano kati ya watu, kutumia ipasavyo uwezo wa ushirikiano na kuendeleza urafiki wa Jamhuri ya Korea na China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma