Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China ahimiza makampuni ya China na UAE kutumia vizuri fursa mpya za ushirikiano
(CRI Online) Septemba 14, 2024
Waziri Mkuu wa China Bw. Li Qiang aliyeko ziarani katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Alhamisi alitoa wito wa kutaka makampuni ya China na UAE kutumia vizuri fursa mpya za ushirikiano chini ya jitihada za pamoja za kithabiti za nchi hizi mbili.
Li alisema hayo alipohutubia Kongamano la Viwanda na Biashara la UAE na China. Alisema uhusiano kati ya China na UAE uko katika kipindi muhimu cha kihistoria, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi mbili unakaribisha fursa muhimu ya kuboreshwa. Anataka makampuni ya nchi mbili yafuate mwelekeo mkuu na kutumia fursa mpya za ushirikiano.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma