Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa zamani wa Ethiopia asema ushirikiano wa karibu zaidi na China unaleta manufaa?kwa pande zote
Abiria wakiwa wameketi kwenye treni katika stesheni ya Nagad kwenye reli ya Ethiopia-Djibouti huko Djibouti, Septemba 19, 2022. (Xinhua/Dong Jianghui)
ADDIS ABABA - "China ni rafiki kwetu. Serikali ya China na watu wake wametoa fursa nyingi barani Afrika, na nia ni kupata manufaa kwa pande zote," Hailemariam Dessalegn, waziri mkuu wa zamani wa Ethiopia, amesema katika mahojiano maalum ya hivi karibuni na Shirika la Habari la China, Xinhua.
Dessalegn amesema kuwa uhusiano wa kihistoria na wa kudumu kati ya China na Ethiopia na bara zima la Afrika umepitia hali mbalimbali kwa miaka mingi na kuwa ushirikiano wa kunufaishana wa "hali zote".
Amesema kuwasiliana na viongozi wa China "kumenifunza mengi kuhusu jinsi Wachina wanavyoangalia mambo kwa makini na kwa tahadhari na kuweza kukabiliana na mambo yote mbaya na mazuri."
Dessalegn amesisitiza mambo yanayofanana ya pande hizo mbili zenye ustaarabu, akisema kuwa Ethiopia na China zina uhusiano wa kihistoria ambao zinaheshimiana na zenye matarajio ya pamoja.
Uhusiano kati ya pande hizo mbili umeshuhudia hatua mpya katika miaka ya hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na Ethiopia kujiunga kwenye BRICS, ikiashiria kuongezeka kwa umuhimu wa Nchi za Kusini, amesema.
Oktoba 2023, China na Ethiopia zilitangaza kupandisha hadhi ya uhusiano kati yao na kuwa ushirikiano wa kimkakati wa hali zote wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed mjini Beijing. Abiy pia alihudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika.
Dessalegn amesisitiza umuhimu wa ushiriki wa China katika maendeleo jumuishi ya kijamii na kiuchumi ya Ethiopia, ambao unajumuisha maendeleo thabiti ya miundombinu na ujenzi wa uwezo wa Waethiopia, haswa miongoni mwa vijana wa nchini humo.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, ambaye alikuwa mjini Beijing kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) na ziara rasmi, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Septemba 5, 2024. (Xinhua/Rao Aimin)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma