Lugha Nyingine
Niger yazindua kampeni ya kupunguza mbu
Mamlaka ya mji wa Niamey, ambao ni mji mkuu wa Niger imetoa taarifa ikisema, mji huo umezindua kampeni ya udhibiti wa mbu inayolenga kupunguza kuzaliana kwa mbu wanaoeneza ugonjwa wa malaria.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa ugonjwa wa malaria umeenea sana katika maeneo yasiyo safi na yaliyo nyuma kiuchumi.
Ili kukabiliana na tishio hilo, viongozi wa mji huo wamehimiza wakazi wa mji huo kuchukua hatua za lazima ya kujikinga, ikiwemo kulinda mahitaji yao ya chakula na vinywaji wati wa kazi ya timu hizo za kutekeleza kampeni hiyo.
Ugonjwa wa malaria unaenea kwa mwaka mzima katika maeneo yote ya vijiji na miji nchini Niger. Kwa mujibu wa maofisa wa huko, ugonjwa huo ni moja ya vyanzo vya udumavu na vifo haswa kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano na wajawazito.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma