Lugha Nyingine
China kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika katika kuondoa mabomu yaliyofukiwa?ardhini barani humo
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Mao Ning amesema China iko tayari kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika katika juhudi za kuondoa mabomu yaliyofukiwa na kuachwa ardhini katika bara hilo na kusaidia kukomesha tishio la mabomu hayo ya ardhini haraka iwezekanavyo kupitia njia mbalimbali zikiwemo misaada ya vifaa, mafunzo ya wafanyakazi, na mwongozo wa eneo la kazi.
China imetangaza “hatua ya Afrika isiyo na mabomu ya kufukiwa ardhini” katika mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika wa mwaka 2024, ambayo ni kati ya hatua mbalimbali za kutekeleza Pendekezo la Usalama Duniani barani Afrika.
Bi. Mao amesema China imechukua hatua halisi kuzisaidia Ethiopia, Angola, Eritrea, Chad na nchi nyingine nyingi kuendeleza uwezo wa kuondoa mabomu hayo ya ardhini, kuchangia katika ulinzi wa usalama wa raia wao na kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nchi hizo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma