Lugha Nyingine
Mamlaka ya uhifadhi wa wanyamapori Tanzania yarudisha mbugani tembo 500 waliovamia makazi?ya watu
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imerudisha mbugani tembo karibu 500 waliovamia maeneo ya makazi ya watu kati ya Januari 2023 na Julai 2024.
Ofisa wa TAWA Bw. Isaac Chamba, amesema tembo hao walirudishwa kwenye makazi yao kwa kutumia helikopta baada ya kuvamia na kuharibu mazao na hata kuua watu.
Amesema tembo hao walifanya uvamizi huo katika wilaya za Nachingwea na Liwale mkoani Lindi, Bunda mkoani Mara, Same mkoani Kilimanjaro, Mvomero mkoani Morogoro, na Mbarali mkoani Mbeya.
Mwezi Mei mwaka huu Wizara ya Maliasili na Utalii ya Tanzania ilitangaza hatua za kudhibiti migongano kati ya binadamu na wanyamapori, hasa mashambulizi ya tembo. Wizara hiyo pia imesema itachukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuajiri walinzi wa wanyamapori 1,187 katika miaka miwili ijayo ili kudhibiti wanyamapori kuvamia makazi ya watu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma