Lugha Nyingine
Uganda yachaguliwa kuwa mwenyeji wa mashindano ya kimataifa ya mchezo wa Kriketi
(CRI Online) Septemba 09, 2024
Uganda imechaguliwa kuwa mwenyeji wa ligi ya Kimataifa ya mchezo wa Kriketi (lCC) kuanzia Novemba 4 hadi 16 mjini Kampala na Entebbe.
Ligi hiyo ya ngazi B ni hatua ya kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia kwa mwaka 2027, zitakazofanyika Zimbabwe, Afrika Kusini na Namibia.
Ofisa Habari wa Chama cha Kriketi cha Uganda (UCA) Denis Musali amesema Uganda inafurahia kuchaguliwa tena kuwa mwenyeji wa mashindano mengine ya kimataifa, ambayo licha ya kuwapa faida ya kuwa waandaaji, pia inaendelea kuisaidia Uganda kuboresha jinsi ya kuandaa michezo mikubwa.
Ligi ya ngazi B itazijumuisha Uganda, Tanzania, ltalia, Bahrain, Singapore na Hong Kong, ambazo zitacheza michezo 15 katika raundi tatu kati ya mwaka 2024 na 2026.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma