Lugha Nyingine
Wataalamu wakutana Kenya kuboresha matumizi ya teknolojia za mambo ya fedha katika kuchochea biashara ndani ya Bara la Afrika
Wataalamu wamekutana katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, kujadili njia za kutangaza suluhu za matumizi ya teknolojia za mambo ya fedha ili kuboresha biashara ya ndani ya Bara la Afrika.
Mkutano wa 11 wa Teknolojia za Mambo ya Fedha wa Afrika umekutanisha washiriki zaidi ya 200 wakiwemo maofisa waandamizi wa serikali na sekta ya huduma za kifedha kutoka Afrika ili kutathmini njia za kupanua matumizi ya teknolojia za kidijitali katika kuimarisha biashara kati ya nchi za Afrika.
Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Eneo la Biashara Huria la Afrika (AfCFTA) Wamkele Mene, amesema teknolojia za mambo ya fedha ni moja ya njia za kuongeza kiwango cha mafungamano ya kibiashara ndani ya Afrika, ambayo inakadiriwa kuwa ni asilimia 15 ikilinganishwa na asilimia 70 ya Umoja wa Ulaya na asilimia 60 barani Asia.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Kidijitali nchini Kenya, John Tanui, amesema teknolojia za mambo ya fedha zinatoa fursa nyingi kuliko utaratibu wa kawaida wa kibenki kutokana na kuwa na suluhu za kiuvumbuzi za kidijitali zinazowezesha malipo ya papo kwa hapo ya kuvuka mipaka.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma