Lugha Nyingine
Marais wa China na Mali wakutana Beijing, kuinua uhusiano wa nchi hizo mbili
(CRI Online) Septemba 04, 2024
(Picha na Ju Peng/Xinhua)
Rais Xi Jinping wa China tarehe 2 Jumatatu amekutana na Rais wa Mali Assimi Goita, ambaye yuko Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).
Viongozi hao wawili kwa pamoja wametangaza kuinua uhusiano baina ya nchi hizo mbili hadi kuwa wa ushirikiano wa kimkakati.
Katika mkutano huo, Rais Xi amesema China inapenda kukuza urafiki wa jadi na Mali, kuendelea kusaidiana kithabiti, na kutoa msaada kadiri ya uwezo wake kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi ya Mali na kuboresha maisha ya watu.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma