Lugha Nyingine
Rais Samia Suluhu wa Tanzania kuongoza mkutano wa mawaziri zaidi ya 70 wa Umoja wa Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS)
(CRI Online) Septemba 03, 2024
Rais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza mawaziri zaidi ya 70 kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS), watakaokutana nchini Tanzania kujadili masuala mbalimbali ya uchumi wa bluu ili kuweka mkakati wa pamoja wa kuimarisha sekta ya uvuvi.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania Bw. Abdallah Ulega, amewaambia wanahabari kuwa mkutano huo utafunguliwa na Dk. Samia Suluhu Hassan Septemba 11 na umepangwa kufanyika sambamba na Kongamano la Kimataifa linalohusu mikakati ya Uboreshaji wa Mnyororo wa Uzalishaji wa Vyakula vya Majini ulioandaliwa na Serikali ya Tanzania, kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Shirika la Chakula Duniani (FAO).
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma