Lugha Nyingine
China yatoa ripoti kuhusu “Ukanda Mmoja, Njia Moja”
(CRI Online) Agosti 30, 2024
Kamati Kuu ya Maendeleo na Mageuzi ya China leo imetoa ripoti ya mwaka 2024 kuhusu maendeleo ya ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.
Ripoti hiyo inaonesha kuwa hadi sasa nchi 52 za Afrika na Umoja wa Afrika zimesaini makubaliano na China kuhusu ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.
Pia ripoti hiyo imesema, mashirika ya China yamejenga au kukarabati zaidi reli zenye urefu wa kilomita elfu 10 , barabara za kilomita 100,000, kujenga madaraja karibu 1,000, bandari 100, mtandao wa umeme takriban kilomita 66,000 na mtandao wa mawasiliano ya habari takriban kilomita laki 1.5.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma