Lugha Nyingine
China yapenda kushirikiana na Afrika kuanza safari mpya ya mambo ya kisasa
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Lin Jian amesema upade wa China ungependa kushirikiana na upande wa Afrika kufunga safari mpya ya kufikia mambo ya kisasa na kutoa mchango kwa pamoja kwa ajili ya kuhimiza mambo ya kisasa ya dunia na maendeleo ya pamoja ya binadamu.
Msemaji Lin Jian ameyasema hayo kwenye mkutano na wanahabari wakati alipojibu maoni ya wataalamu na wasomi wa Afrika kwamba China kwa ushirikiano wake na Afrika kweli itaisaidia kwa njia ya kiafrika ili bara hilo lifikie mambo ya kisasa? Na wamesema, pande hizo mbili zinatakiwa kushirikiana katika njia zao za kuleta maendeleo ya mambo ya kisasa.
Msemaji huyo akisema kuwa kutimiza mambo ya kisasa ni utafutaji wa pamoja wa China na nchi za Afrika, China inaunga mkono kithabiti Afrika katika kutafuta njia ya maendeleo kwa kujiamulia na kutilia mkazo maeneo matatu ya dharura yanayohitajika kwa kuhimiza mambo ya kisasa ya Afrika. Na chini ya mfumo wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), upande wa China umeanzisha Mpango wa Kusaidia Maendeleo ya Viwanda barani Afrika, na kutekeleza Mpango wa China Kusaidia Maendeleo ya Kilimo barani Afrika na Mpango wa Ushirikiano kati ya China na Afrika wa Maendeleo ya kuwaandaa watu wenye ujuzi ili kusaidia maendeleo ya Afrika na ustawi kwa hatua madhubuti.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma